Peniela Season 1 Sehamu ya Kwanza - STORY ZA MAPENZI

Peniela Season 1 Sehamu ya Kwanza

Simulizi : Peniela (Story Ya Kijasusi)Sehemu Ya Kwanza (1)


Ni saa sita za usiku sasa bado jaji Elibariki chukuswa yuko sebuleni akiendelea kupitia kitabu chake cha sheria .Katika meza ndogo kulikuwa na vitabu vingine zaidi ya saba vya sheria.Aliendelea kufungua ukurasa baada ya ukurasa.Alionekana kuwa na mawazo mengi mno.Wakati akiendelea kupitia kurasa za kitabu kile mke wake akaingia pale sebuleni akiwa na kikombe cha kahawa, akakiweka mezani halafu akainama na kumbusu mumewe.

“ You need to take a rest now.Tommorow is your big day” akasema Flaviana mwanamke mwenye uzuri wa kipekee.Elibariki akakifunika kitabu chake na kumtazama mkewe ,akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo na kusema

“ Natamani sana nipumzike lakini sina hakika kama nitapata usingizi.”
Mke wake akamuangalia kwa makini halafu akasema
“ Kuna jambo nataka nikuulize mume wangu”
“ Uliza usihofu ”
“ Najua kesi hii ni moja kati ya kesi kubwa na ngumu kwako.Hukumu unayotarajia kuitoa kesho inasubiriwa kwa hamu kubwa sana na umma wa watanzania.Wewe ni jaji na nina imani maamuzi yako utakayoyachukua ni sahihi kabisa,lakini swali langu ni je Yule msichana ana hatia?
Swali lile lilionekana gumu sana kwa jaji Elibariki.Akainama akafikiri kidogo halafu akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo na kumtazama mkewe.

“ My love kesi hii ni ngumu sana na imejaa utata mwingi na ndiyo maana unaniona mpaka hivi sasa bado niko hapa.” Akasema Elibariki
Flaviana akamtazama mume wake na akagundua kwamba hakuwa tayari kumjibu swali alilouliza.Akas
imama na kusema

“ Sina wasi wasi na maamuzi utakayoyatoa kesho lakini nakuomba utoe haki kwa upande wenye haki.”
Elibariki hakumjibu kitu akabaki akimuangalia
“ Come to bed when you are done,but don’t stay till very late.You have a big day tomorrow.” Akasema Flaviana na kuelekea chumbani .Elibariki akavuta pumzi ndefu na kuchukua kitabu chake cha sheria akaendelea kukisoma.
“ Katika maisha yangu ndani ya sheria sijawahi kukutana na kesi ngumu yenye mitihani kama hii.Hata hivyo niliapa kusimamia sheria na kutenda haki kwa kila mwenye haki.

Katika maamuzi yangu ya kesho lazima nifanye kwa haki japokuwa nina hakika nitakuwa katika matatizo makubwa baada ya hukumu ya kesho lakini siwezi kupindisha sheria eti tu kwa sababu ya shinikizo toka kwa mtu au kikundi cha watu.Mungu ataniongoza na kunisimamia ili nitoe hukumu ya haki” akawaza Elibariki na kufunga vitabu vyake akaelekea chumbani kulala.tayari Flaviana mke wake amekwisha lala.Akamtazama kwa makini na kujisemea moyoni

“ Nina hakika hata wewe hautanitazama vizuri baada ya hukumu ya kesho,lakini sina namna nyingine zaidi ya kutenda haki.Utanisamehe mke wangu” akawaza Elibariki na kupanda kitandani kulala.

***********

“ Eli my love,amka kumekucha !! ..Ilikuwa ni sauti tamu na laini ya Flaviana akimuamsha mumewe.Jaji Elibariki ambaye asubuhi hii alionekana kuzama katika usingizi mzito akafumbua macho huku akiguna na kutazama saa ya ukutani.Ni saa kumi na mbili na dakika ishirini za asubuhi.
“ jana sikupata usingizi kabisa.Usiku wangu ulikuwa mrefu sana” akasema kwa sauti ya uchovu.

“ Please wake up honey.Today its going to be a very long day” akasema Flaviana.Elibariki akainuka na kuelekea katika chumba chake cha mazoezi akafanya mazoezi kidogo halafu akaelekea bafuni.Bado kichwa chake kiliendelea kuwa na mawazo mengi sana.Kisha oga akarejea chumbani na kukutana na suti nzuri aliyoandaliwa na mke wake akavaa na kujitazama katika kioo kikubwa kilichokuwamo chumbani mwao.Aliganda pale katika kioo hadi mke wake alipoingia naye akaanza kujiandaa.

“ Leo unakwenda kazini? Akauliza Jaji Elibariki.Flaviana akacheka kidogo na kusema
“ Usinichekeshe mume wangu,yaani niende kazini leo? Siwezi kufanya hivyo hata kidogo.Leo ni siku yako kubwa.Ni siku yetu kubwa.Ni siku ambayo jina lako litaingia katika vitabu vya historia kwa hukumu unayokwenda kuitoa.Vyombo vyote vya habari vitakuwepo mahakamani ,lazima na mimi niwepo nikuunge mkono pamoja na mdogo wangu Anna.” Akasema Flaviana.Elibariki hakujibu kitu akaendelea kujitazama katika kioo.

“Are you nervous my love? Akauliza Flaviana
“ No I’m not” akajibu Elibariki halafu wakaongozana kuelekea katika chumba cha chakula kwa ajili yakupata kifungua kinywa.Wakati wakiendelea na kupata kifungua kinywa simu ya Jaji Elibariki ikaita.Akaitazama ikiita akasita kuipokea.
“ Mbona hupokei hiyo simu? Akauliza Flaviana
“ Its your father.Mr President” akajibu Elibariki
“ Usiogope.Ongea naye .Si kawaida yake kupiga simu mida kama hii.Inawezekana ana jambo la maana la kukwambia” Akasema Flaviana.Elibariki akaichukua simu na kubonyeza kitufe cha kupokelea huku akiinuka na kuelekea sebuleni.

“ Hallo Mr President” akasema Jaji Elibarki
“ Hallo Jaji.Mnaendeleaje vijana wangu?
“ Tunaendelea vizuri mzee.Ninyi mnaendeleaje?
“ Tunaendelea vizuri sana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Nashukuru kusikia hivyo” akasema Elibariki na kimya kifupi kikapita
“ Elibariki,today its your big day” akasema Mheshimiwa rais.
“ Najua unakwenda kutoa hukumu katika kesi ngumu inayovuta hisia za watu wengi na hasa kwa kuwa binti wa rais naye kesi hii inamuhusu kwani mchumba wake ndiye aliyeuawa.Sikufundishi kuifanya kazi yako lakini fanya maamuzi ya haki kwa namna uonavyo wewe.Pamoja na hayo kuna jambo ambalo nataka kukuomba kijana wangu” Akasema Dr Joshua Johakim rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“ Nakusikiliza mzee” akasema Jaji Elibariki kwa wasi wasi .
“ Nilikuteua kuwa jaji kwa sababu wewe ni msomi mzuri na unazifahamu sheria za nchi kwa hiyo sitaki kuingilia maamuzi yako lakini nakuomba kijana wangu,try in anyway you can to make my daughter Happy.Alimpenda sana Edson.Ni hilo tu ninalotaka kukuomba kijana wangu.Nakutakia siku njema” akasema mheshimiwa rais na kukata simu.Jaji Elibariki alibaki ameduwaa asijue afanye nini.Maneno yale ya rais ambaye ni baba mkwe wake yalimfanya ahisi kuchanganyikiwa.

“ Huu ni mtihani mgumu sana lakini Mungu atanitangulia nitatenda haki” akawaza Elibariki na kurejea mezani
“ Amekwambia nini baba? Mbona sura yako imebadilika namna hiyo? Akauliza Flaviana
“ Nothing.Just greetings” akajibu Elibariki na kuendelea kupata kifungua kinywa.Baada ya kumaliza akarejea chumbani na kujitazama tena katika kioo na kuvuta pumzi ndefu.

“ Please help me Lord.I’m in a very difficult situation” akasema Elibariki kwa sauti ndogo na mara mke wake akaingia mle chumbani
“ Its time my love.Are you ready?
“ Let’s go” akasema Elibariki ,wakatoka wakaingia garibni na kuondoka.

**********

Hakukuwa na nafasi tena ya kukaa ndani ya chumba cha mahakama kutokana na watu kujaa.Ni siku ya hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili mmiliki wa maduka makubwa ya mavazi ya Penny Fashion,Peniela Salimote.Kesi hii iliyovuta hisia za watu wengi na kuwafanya wafurike ili kuja kusikia hukumu ilikuwa inaonyeshwa moja kwa moja katika runinga.ILikuwa ni kesi ya kwanza kubwa kurushwa moja kwa moja katika runinga.Katika kila kona ya nchi watu walikuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya kesi hii ambayo hukumu yake ilikuwa inasubiriwa na watu wengi.

Ndani ya chumba cha mahakama ilikuwepo familia ya rais ikiongozwa na mke wa rais,Dr Flora Johakim ambaye alikuwa ameambatana na binti zake wawili Flaviana na Anna.Familia ya Edson Kobe kijana anayedaiwa kuuliwa na Peniela nayo ilikuwepo mahakamani hapo ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka.Familia ya Edson na ile ya rais zilikuwa ni familia rafiki kwa muda mrefu sana.Kwa upande wa Penny hakukuwa na ndugu yake yeyote aliyefika mahakamani pale zaidi ya rafiki zake wachache.

Tayari mtuhumiwa amekwisha ingizwa mahakamani na aliyekuwa akisubiriwa ni jaji anayeisikiliza kesi ile aweze kuingia na kuisoma hukumu.Wakati wakimsubiri Jaji aingie,Jason Patrick mwanasheria anayemtetea Penny alikuwa akibadilishana mawili matatu na mteja wake .
“ Jason,kabla hukumu haijaanza ninaomba nikwambie kitu.” Akanyamaza kidogo na kuendelea.

“ Nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.Umenisimamia katika kesi hii kwa kila namna ulivyoweza.Najua chochote kinaweza kikatokea siku ya leo hivyo nakuomba endapo ikitokea nikakutwa na hatia na kufungwa kifungo cha maisha au kifo uhakikishe yale yote niliyokuandikia katika karatasi unayatimiza.Wewe ni zaidi ya rafiki.Wewe ni ndugu yangu pekee ninayekutambua.Ninakukabidhi kila kilicho changu endapo mambo yataenda kinyume na matarajio yetu." Akasema Penny huku machozi yakimtoka
“ Penny naomba usikate tamaa hata kidogo.Nimepambana vya kutosha kuhakikisha kwamba tunashinda kesi hii lakini kama mambo yataenda tofauti na matarajio yetu hautakuwa ni mwisho.Nitapambana hadi nihakikishe haki imepatikana.” Akasema Jason na mara jaji akaingia.

Wakati Jaji akiingia Penny akamnong’oneza Jason sikioni
“ I didn’t do it.I didn’t kill him”
“ I know Penny and I believe you” akasema Jason na mara mahakama ikaanza.”


Masaa manne yamekwisha katika sasa toka Jaji Elibariki alipoanza kuisoma hukumu .Ndani ya chumba cha mahakama kulikuwa na ukimya mkubwa kila mtu akifuatilia kwa umakini mkubwa kila alichokisema Jaji.Baada ya maelezo marefu kuhusiana na mwenendo mzima wa kesi ,hatimaye ukafika wakati wa kuhitimisha hukumu,wakati ambao ni mgumu kwa kila mtu mle mahakamani.Mke wa rais Dr Flora Joakin alishikana mikono na wanae Flaviana na Anna wakipeana moyo.Familia ya Edson halikadhalika walikuwa katika wasi wasi mkubwa kwani hakuna aliyejua jaji anakwenda kusema nini.

Toka alipoingia ndani ya chumba cha mahakama,Anna mtoto wa rais amekuwa akimtazama kwa hasira Peniela aliyekaa ndani ya kizimba kilichokuwa mbele kabisa ya mahakama.

“ Leo ndiyo siku yako ya mwisho kahaba wewe,mdanida waume za watu.Ndani ya muda mfupi ujao utayaanza maisha mapya gerezani paka wewe.Nilikuahidi kwamba utaozea gerezani na sasa utayaamini maneno yangu.Mwangalie kwanza alivyopauka na kukondeana kama muwa.” Akawaza Anna akiendelea kumtazama Penny kwa hasira
“ Ulinitenganisha na Edson mwanaume niliyempenda kuliko wote duniani.Urafiki wetu ulianza toka utotoni lakini ulivuruga kila kitu na mwishowe Edson akaniacha.Ninakuchukia wewe mwanamke na na laiti ningekuwa na uwezo ningekukata masikio “ Anna aliendelea kuwaza na akashindwa kuyazuia machozi kumtoka .Kitendo cha kumuona tena Peniela kilimrejeshea taswira ya Edson mwanaume aliywahi kumpena kupindukia.Akainama na kufuta machozi

Wakati kila mtu moyo ukimuenda mbio akisubiri maamuzi ya Jaji,Peniela alikuwa amefumba macho michirizi ya machozi ikionekana mashavuni pake.Alikuwa akiomba.

“ Ee Mungu baba,wewe ndiye mwenye uwezo wa kuona kila kitu hadi ndani ya mioyo yetu.Baba unafahamu sijatenda kosa hili ninaloshtakiwa nalo.Nimeteseka gerezani kwa mwaka mzima na hakuna anayeonekana kuniamini kwamba sikumuua Edson.Baba imetosha sasa na ninaomba kwa mapenzi yako itolewe hukumu ya haki”
Jason mwanasheria wake alikuwa amemuelekezea macho akimtazama na kumuonea huruma sana.

“ She’s Innocent.She didn’t kill him.Please Lord help her” akawaza Jason.Penny aliendelea kuyafumba macho yake machozi yakiendelea kumtoka na mikono yake akiwa ameifumbata kifuani .Jaji Elibariki aliendelea kumalizia kuisoma hukumu yake
Taratibu Penny alihisi miguu yake inaisha nguvu pale Jaji alipotamka kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kuithibitishia mahakama kwamba Penny alimuua Edson licha ya kuwasilisha ushahidi na vielelezo vingi.Jaji Elibariki alikwenda mbali zaidi na kuainisha namna ushahidi uliotolewa mahakamani ulivyokosa nguvu ya kuweza kumtia hatiani mshtakiwa kwa hiyo kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa anamuachia huru Penny.Alipotamka tu maneno hayo Penny akaanguka na kupoteza fahamu.

**********

Mtu wa kwanza kumtambua baada ya kurejewa na fahamu akiwa hospitalini alikuwa ni Jason mwanasheria wake.Mara tu alipopoteza fahamu baada ya Jaji kumuachia huru ,Penny alikimbizwa katika hospitali ya karibu kwa ajili ya huduma ya kwanza.

“ Jason ..!.akasema Penny kwa sauti dhaifu huku akitaka kuinuka lakini akashindwa mwili haukuwa na nguvu.
“ Penny relax ..!!!..Endelea kupumzika…” kabla hajamaliza sentensi yake Penny akapoteza tena fahamu.

“ Amepatwa na mstuko mkubwa huyu binti.Tunahitaji kumuweka hapa kwa muda tuendelee kumuangalia” akashauri daktari.
Jason Patrick mwanasheria anayemtetea Penny hata naye bado alikuwa katika kutoamini kama ni kweli Penny ameachiwa huru.Alifanya kazi kubwa ya kumtetea Penny lakini ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ulikuwa mzito na uliotosha kabisa kumtia hatiani mteja wake.

Alimshukuru Mungu kwa muujiza ule mkubwa.Alimshuk
uru vile vile jaji Elibariki kwa maamuzi yale ya haki.
“ Haki imetendeka.Jaji Elibariki ameweka historia kwa kutoa hukumu ambayo wengi hawakuitegemea” akawaza Jason na mara daktari akamfuata na kumwambia kwamba kuna kundi la waandishi wa habari nje wanaohitaji kuongea na Penny.Akatoka na kwenda kukutana nao na kuwataarifu kwamba Penny hakuwa tayari kuongea na waandishi wa habari kwa wakati huo.

**********

Jaji Elibariki alipomaliza kutoa hukumu yake akatoka ndani ya mahakama huku nyuma yake akiacha vilio na mshangao kwa wengi hasa wale wa upande wa Edson.Asilimia kubwa ya wale waliokuwa waki fuatilia kesi ile waliamini kwamba lazima mahakama ingemkuta na hatia Penny. Flaviana mke wa Jaji Elibariki alikuwa amesimama amejishika kiuno asiamini kile kilichokuwa kimetokea

“ How could you do this to us Eli…!! Akasema kwa sauti ndogo na kupandwa na hasira alipomtazama mdogo wake Anna ambaye alikuwa ameanguka chini ameishiwa nguvu .Familia ya Edson nao hawakuamini kilichokuwa kimetokea.Walik

umbatiana na kulia kwa pamoja .Hawakuamini kama ni kweli mtu anayesadikiwa kumuua mtoto wao ameachiwa huru.
Dr Flora Joakim mke wa rais akakumbatiana na mama wa Edson na kumfariji akimuhakikishia kwamba huo haukuwa mwisho.Watapambana hadi haki ipatikane.


******** ***********
Itaendelea..................