Nauza Bikira Yangu: Sehemu Ya Kwanza
May 28, 2020
Edit
Simulizi : Nauza Bikira Yangu
Sehemu Ya Kwanza (1)
NAUZA BIKIRA YANGU
11/8/1964
Msafara wa magari yapatayo zaidi ya 40 ukiwa unaongozwa na pikipiki za polisi wa usalama wa barabarani, Ukifuatiwa na magari ya polisi kisha magari ya viongozi waandamizi wa nchi, katikati
gari la Rais Elibariki Chalambo Maarufu kama Chalambo Rais wa Jamuhuri ya watu wa KOLO nchi iliyo kaskazini mwa Tanzania. Wananchi wenye matuini na Rais Chalambo walikuwa wamejipanga Barabarani wakiwa na Bendera za nchi hiyo huku wakiimba nyimbo za furaha za kulitukuza taifa la Jamuhuri ya Kolo na Rais wao Chalambo. Rais Chalambo akiwa na mke wake Tclee katika gari la wazi huku akiwapungia wananchi mkono, Masafara unaishia ndani ya uwanja wa Uhuru ulioko katika jiji la Pona moja ya majiji makubwa katika nchi ya Kolo.
Akipokewa na halaiki ya watoto, huku akiwa mwenye furaha anafungwa skafu kisha anakagua Gwaride la Jeshi la wananchi wa Kolo, Kwa mwendo wa kikakamavu anaelekea katika eneo rasmi lililotengwa katka jukwaa kuu anakaa. Mshehereshaji wa Sherehe za Uhuru wa nchi hiyo wa siku hiyo alikuwa ni mwanajeshi wa jeshi la kujenga taifa na mwimbaji wa bendi ya jeshi ya nchi hiyo aitwae Alkad. Kwa mbwembwe na vibwagizo anatoa nafasi kwa Katibu mkuu wa serikali ya Kolo ambae ndiye mwenye jukumu la kutambulisha viongozi mbalimbali wa serikali na viongozi wa mataifa mblimbali waliohudhuria sherehe hizo.
"Naomba sasa nimuite kwenu, Jemedari, Kiongozi, Mnyenyekevu na Mtendaji wa serikali mwenye jukumu la kuwatambulisha viongozi hapa leo, Si mwinine ni Katibu mkuu wa Jamuhuri ya Kolo, Muheshimiwa Suddy Mnyamwezi" Makofi na kelele vintawala.
Kijana mwenye umri kati ya miaka arobini mpaka arobaini n tano aliyevalia suti yake nadhifu ya rangi ya kijivu, Kwa ukakamavu huku uso wake ukipambwa na Tabasamu anasogelea kipaza sauti mkononi akiwa kashika karatasi nyeupe, Akilegeza koo kwa kukohoa kikohozi kidogo anaanza kuongea.
"Muheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya watu wa Kolo, Waheshimiwa viongozi mbalimbali, Waheshimiwa wananchi wa Jamuhuri wa watu wa Kolo, Napenda kuwakaribisha katika sherehe za miaka ishirini na moja toka nchi yetu kupata uhuru na kuchaguliwa kidemokrasia." Suddy anageuka na kuangalia wananchi wakipiga makofi ya nguvu huku wakiwa na nyuso zenye matumaini.
"Naomba nichukue nafasi hii kutambua uwepo wa Mkuu wa majeshi ndani ya jamuhuri ya watu wa Kolo Kanal NGWALI naomba asimame apunge mkono kwa wananchi" Mzee mwenye mvi nyingi kichwani akiwa kavalia mavazi ya Jeshi yenye nyota nyingi mabegani anasimama na kupiga saluti akimuelekea Rais Chalambo kisha anakaa.
"Naomba nimtambulishe kwenu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya watu wa Kolo Mh, Bony Sadoti," Kijama mwenye mwili wa mazoezi akiwa kavalia kaunda suti nyeusi iliyomkaa vyema anasimama na kupunga mkono kila upande huku akitabasamu, Kelele za kushangiliwa zinasikika.
"Sasa naomba niwasimamishe mawaziri wa wizara mbalimbali katika Jamuhuri ya watu wa Kolo." Kundi la watu waliokaa mstari wa nyuma baada ya mstari wa mbele aliokaa rais, Wanapunga mikono na kuketi.
"Naomba sasa nitambue uwepo wa Rais wa Tanzania, Rais wa Gambia, Rais wa Kenya, Rais wa Uturuki, Rais wa Ufaransa, Rais wa Zimbabwe, Rais wa Nigeria na Rais wa Uganda, Naomba wasimame na kusalimu wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo. Kundi la Marais wa nchi mbalimbali linasimama na kupunga mkono huku Kikosi cha brass band cha jeshi kikipiga ala za muziki.
"Wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo naomba sasa nimkaribishe Rais wetu Mh Chalambo azungumze nanyi"
Kelele za shangwe na vigelegele zinasikika. Akiwa na sura isiyo na furaha huku akiwa makini kutazama karatasi iliyo mezani kwake Rais Chalambo anasimama na kuanza kuongea.
"Mlinichagua ili niwatumikie kwa uaminifu, Na leo ikiwa ni siku muhimu kwa Tiafa letu, Baba zetu na babu zetu walipigana na kufa kwa ajili ya nchi yetu, Maelfu ya ndugu zetu walikufa kwa ajili ya kupigania uhuru na nchi hii iwe huru, na tarehe kama ya leo miaka ishirini iliyopita wakafanikiwa kuikomboa nchi hii katika mikono ya wakoloni, Leo nataka kuitoa nchi yenu katika mikono ya watu wachache" Kimya kinatawala, Mawaziri wanaonekana wakiangaliana, Mkuu wa Jeshi kanal Ngwali anaonekana yuko makini kuandika ujumbe katika sinu yake ya kiganjani. Kwa sauti isiyo na mzaha Rais Chalambo anaendelea kuzungumza.
"Mimi nikiwa kama Amiri Jeshi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo na Rais niliyechaguliwa kwa kura za wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo natangaza Rasmi Baraza la Mawaziri limevunjwa na Jeshi liko chini yangu na Hakuna Mkuu wa Majeshi namaanisha Kanal Ngali si kiongozi wa Jeshi mpaka pale nitakapotangaza Rasmi" Maamuzi yenye maneno ya kuamrisha yalimtoka Rais Chalambo na kupokewa na sauti za Kushangilia toka kwa Wananchi wakikubaliana na Maamuzi ya Rais wao. Mawaziri walisimama na kuondoka meza kuu huku Mkuu wa Majeshi akivua Mkanda, Kofia na Shatu lenye nyota za jeshi kisha anaweka juu ya kiti na kuondoka.
"Ni bora kubaki na watu wachache watakao tumikia nchi na wananchi kwa uadilifu kuliko kuwa na kundi kubwa la wanyonyaji natangaza Rasmi nchi hii sasa ni huru kwa mara ya pili." Rais Chalambo aliongea kwa sauti ya kishujaa iliyopokewa kwa kelele za shangwe toka kwa wananchi wake. Mizinga na Fataki vilipigwa juu kama ishara ya kufunguliwa kwa sherehe za uhuru wa nchi hiyo.
********** ************
Katika chumba chenye mwanga hafifu mbele ya meza ya Duara kundi dogo la watu waliokaa katika viti wakiwa na nyuso zenye hasira na mawazo tele walikua wakijadili jambo kwa umakini.
"Hii haiwezekani, Tumuweke sisi katika nafasi ile leo atuaibishe mbele ya wananchi, This is too much" Ngwali alizungumza kwa jazba huku akigongagonga meza kwa ngumi.
"Mkuu ni vyema tukapanga chakufanya maana hili jambo limemuumiza kila mmoja wetu" Paul Bona waziri wa mambo ya nje alizungumza huku akifunbata mikono yake kama anaomba usikivu.
"Mimi napendekeza Tugomee maamuzi yake sababu sisi ni wengi hawezi kutushinda?" Rosemary Antony waziri wa Fedha alitoa mawazo yake.
"Rose hilo wazo lako litapingana na Katiba, Katiba inasema Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuvunja Baraza la mawaziri na pia ndiye mwenye mamlaka ya kuajiri na kufukuza viongozi wa jeshi" Waziri Mkuu alijibu huku akiinamisha kichwa chini kwa kukata tamaa.
"Jamani mimi ninawazo, Huyu Rais wetu anapenda sana wanawake mnaonaje tukamtafutia mwanamke kisha tunamtengenezea skendo tunaitoa katika magazeti na tv tena Mh Deogratias ana magazeti na mimi nina Tv mbili vinatutosha kumchafua, Kwa hiyo skendo tutakua tumepandikiza chuki dhidi yake kwa wananchi halafu tunaanzisha vuguvugu la kumshinikiza ajiuzulu akijiuzulu uchaguzi unafanyika tunamuweka mtu wetu" Waziri wa sheria ndugu Abdallah ally alitoa wazo lililopingwa na Agness Todi Naibu waziri wa Afya.
"Hilo wazo lako si sahihi kumbukeni tukimshirikisha mwanamke mwingine zaidi yetu itakua shida tena ambaye hajaathirika na hili tatizo kweli hilo wazo lako ni zuri ila ni gumu kulitekeleza maana hapo ni lazima washirikishwe na waandishi wa habari huoni hiyo ni hatari?"
"Sasa Tufanyaje" Sauti ya kukata tamaa ilimtoka Ngwali.
Salomenyo chaloo waziri wa ulinzi aliyekua kainamisha kichwa chake chini akiwa kimya anainua kichwa na kuchomoa bastola yake katika pochi na kuruka mpaka mbele na kuwaweka wenzake chini ya ulinzi.
"Laleni chini pumbavuuuuuu" Sauti ya ukali toka kwa Salomenyo inawachanganya na kulala chini kwa woga, Salomenyo anapiga risasi katika ukuta na kurudi kukaa katika kiti chake na kuinamisha kichwa chini. Zinapita dakika kadhaa wale viongozi wanainuka kwa woga huku wakishangaa Salomenyo kakaa kwenye kiti kainamisha kichwa chini kama alivyokuwa mwanzo.
"Hivyo ndivyo tutakavyomdhibiti huyu Rais wenu" Salomenyo aliongea huku kainamisha kichwa chini.
"Sijakuelewa mheshimiwa" Naibu waziri wa Afya Agness Todi alijibu kwa woga.
"Sikilizeni hapa dawa ni kumuua huyu rais kama ninyi mlivyolala chini ndivyo atakavyovamiwa na risasi ziutawanye ubongo wake atuachie nchi yetu yeye aende na uzalendo wake" Salomenyo alijibu kwa sauti ya kutetemesha iliyopokewa na kauli moja toka kwa Ngwali.
"Geneous"
"Sasa nani atafanya kazi hiyo?"swali kutoka kwa Paul Bona lilizua mjadala mrefu na maamuzi yakatolewa kazi apewe mwanadada machachari asiyeogopa kuua na ni mwanajeshi mwenye shabaha mwenye Cheo cha ukoplo latika Jeshi la Wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo si mwingine ni Chiku. Kazi ilitakiwa kufanywa haraka kabla ya sherehe za uhuru kumalizika. Chiku Tayari alikua mbele ya meza yenye viongozi wapatao nane na ahadi ya kupewa urais pindi atakapokamilisha kazi hiyo ilikua ikiutekenya moyo wake na kumpandisha morali wa kukamilisha kazi haraka ili awe Rais wa Kolo.
Bunduki yake aina ya SMG iliyojaa Risasi ikiwa begani, Kombati ya Rangi ya khaki ikiwa imemkaa vyema miwani ya kuzuia Jua na Soksi za kuzuia mikono zikiwa zimevikwa vyema katika mikono yake, Akiwa juu ya pikipiki safari ya kuelekea njia Panda ya kuelekea Toraa mji mdogo wa nchi ya kolo wenye vivutio vingi vya utalii na Machimbo ya madini ghali duniani ya Ramnet na njia ya kuelekea ikulu ya Kolo iliyo pembezoni mwa jiji la Pona.
Breki za pikipiki zilifungiwa mbele ya jumba kuu kuu linalotazamana na barabara hiyi, Chiku akiwa na bubduki yake akatafuta eneo zuri na kukaa huku akivuta sigara taratibu mawazo yake yakifikiria kiti cha urais alichoahidiwa, Sauti za ving'ora ndizo zilimshtua na kukaa vyema huku silaha yake ikiwa mkononi, Utaalamu wake wa kulenga vitu vilivyo mbali ndio uliomfanya kuwa na uhakika wa kukamilisha kazi kwa urahisi. Baada ya pikipiki na magari machache kupita msafara haukua mrefu kwa kuwa haukua na msururu wa mawaziri kama mwanzo macho ya Chiku yakatua katika Gari la wazi alilo[akia Rais na Mkewe.
"Ladies First"
Ni kauli aliyotamka chiku na kuvuta kitufe cha kufyatulia risasi akiwa kamlenga vyema mke wa Rais Chalambo, Bi. Tclee.
********** **************
Wakiwa katikati ya msitu wa pinar del rio ulioko cuba's western katika nchi ya Cuba, Makomandoo wa nne kati ya makomandoo kumi na tano wakiwemo makomandoo saba kati yao wakiwa wametoka katika nchi ya Kolo, Ni zaidi ya miezi nane imekwisha wakihangaika kutoka katika msitu huo wenye simba wengi na nyoka wenye sumu kali aina ya Kobra, Kisu na bastola yenye risasi tatu tu ndivyo vitu pekee walivyopewa kujilinda kwndani ya msitu huo, Mpaka kufika wakati huo makomandoo kumi na mbili walikuwa wameshakufa kwa kuliwa na simba huku wengine wakiumwa na nyoka na wengine wakifa kwa njaa. Ni Ismaeel ahmed kutoka Misri, Berno Mlay kutoka Jamuhuri ya watu wa Kolo na Osi Inieka kutoka Nigeria ndio makomandoo pekee waliobaki katika msitu huo. Damu nyingi zikiwa zinamvuja Osi katika mguu wake wa kulia baada ya kuvamiwa na Simba Risasi yake moja iliyo katika bunduki ndiyo iliyomsambaratisha simba aliyekua kashikilia mguu ule. Akiwa chini ya mti mkubwa kiza kimetawala kwa kutumia tochi aliyoivaa kichwani Macho yake yakakutana na simba mkubwa akija kumfuata alipo, Kwa haraka akajivuta na kushika mti huku akijitahidi kupandisha mguu ili apande ule mti, Maumivu makali kutoka katika lile jeraha yalimrudisha chini na kukutana na kinywa cha Simba na kuruhusu meno makali kushika mfupa wa mguu ule na kuuchana katikati, Kelele kubwa kutoka kwa Osi ilimshtua Berno na kupapasa kisu chake kama kiko sawa akaamka na kujishika vizuri akiwa juu ya mti alipojiegesha katika tawi moja kubwa lililolala kama kitanda. Mngurumo wa simba ulimfanya kujishika vizuri huku akijizuia kwa majani ili asiweze kuona chini, Kupitia upenyo mdogo alishuhudia Simba mkubwa akiwa anavuta mwili wa Osi ukiwa umetapakaa Damu mpaka katika eneo la wazi lenye watoto watano wa simba wakaanza kushambulia ule mwili.
"Dah haya sasa ni mateso ndiyo mafunzo gani haya" Berno aliongea mwenyewe huku akiogopa sauti yake iliyokua akijirudia masikioni mwake.
Huyu ndiye Berno komandoo pekee aliyefuzu mafunzo ya hatari ya ujasusi katika nchi ya Cuba, Ugomvi mkubwa kati ya Serikali ya Africando nchi yenye fedha nyingi na inayosaidia nchi nyingi za afrika iliyo kusini mwa nchi ya Kolo ilivunja uhusiano na Jamuhuri ya watu wa Kolo sababu ya nchi hii kukataa Berno kwenda kufanya kazi katika kitengo cha ujasusi cha nchi hiyo ndicho kitu kilichopelekea Africando kusitisha misaada yake katika nchi ya Kolo baada ya Rais Chalambo kukataa ofa ya Makomandoo kumi kutoka Africando wabadilishane kwa komandoo mmoja tu ambaye ni Berno. Madini ya Ramnet pekee yalitosha kuendesha uchumi wa nchi ya Kolo. Kazi ya kulinda usalama wa nchi na Rais aliyopewa Berno ilimuwezesha kuishi popote alipotaka na kupata huduma yeyote bure ndani ya nchi ya Kolo kwa kutumia G3 Card. Ni Card ambayo anaweza kuchukua kiasi chochote cha fedha katika benki yeyote.
Akiwa katikati ya wananchi ndani ya uwanja wa Uhuru, Jua kali ndilo lililomkimbiza na kuamua kuelekea nje na kutafuta maji, Kila duka aliloenda hakupata huduma kwa kuwa lilikua limefungwa. Mpaka Rais anafunga sherehe na kutoka Tayari Berno alikua katembea umbali mrefu sana.
Mwanamke aliyepaki pikipiki kilometa chache kutoka katika kibaraza cha duka aliliposimama Berno alimvutia na kuhamisha macho yake kwa binti yule. Wasiwasi wa binti yule na kutazama saa mara kwa mara kulimfanya Berno ahisi tatizo na kukaa vyema huku bastola yake aina ya Rivolvo yenye kiwambo cha kuzuia Risasi ikiwa kiunoni huku mkono wake ukilegeza pochi ya kuhifandia bastola ili kuifanya itoke kwa haraka pindi itakapohitajika kufanya kazi. Kama mawazo yake yalivyomwambia ndicho kilichotokea. "Watu wabaya wote duniani huwa na wasiwasi kabla ya kutimiza adhma yao na baada ya kutimiza na hiyo ndiyo njia mojawapo ya kumtambua adui" kauli ya mkufunzi wake Convickie scochxic raia wa Urusi ndiyo ilimfanya Berno atabasamu na kutaka kujua mwisho wa Yule binti.
Baada ya Msafara wa Rais kutokea Chiku akimlenga vyema mke wa Rais Chalambo bi Tclee Jicho la Chiku lilitua kwa kijana aliyesimama pembeni ya kibaraza cha Duka akijifanya haangalii kule alipo, Kama umeme Mdomo wa Bunduki ukahama na Risasi ikaanza kusafiri kutoka katoka chemba ya bunduki na kutokea katika mdomo wa SMG mlio mkubwa ulisikia ambao Berno hakuusikia huku akidondokewa na Tone kubwa la damu na kufanya macho yake kupoteza nguvu ya kuona na kudondoka chini, akiwa juu ya pikipiki Chiku alizungusha pikipiki kama wafanyavyo waendeshaji wa mashindano ya pikipiki na kuingia katika barabara ya vumbi huku akikimbizwa na pikipiki nyingi za polisi, Kwa umahiri wa kucheza na pikipiki tayari alikua mbele ya msafara na Risasi zisizopungua kumi zilikua zimekutana na mwili wa Rais Chalambo pamojba na mkewe huku wakiwa wamekumbatiana na wakati huo Tayari Chiku alikua amekwishatoweka eneo hilo.